Monday, September 30, 2013

NJOO UWE SEHEMU YA HISTORIA HII YA TANZANIA NA JOHN LISU!!

UKO HAPA DVD LIVE RECORDING
 NA JOHN LISSU,
06/10/2013,CCC-UPANGA, DAR ES SALAAM, TANZANIA.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE;
SALAM TANZANIA!

Shalom Dar es salaam, Shalom Tanzania!
Ndugu wanahabari na watanzania wote kwa ujumla!
Naamini tuko salama na tunaendelea na shughuli zetu za kila siku alizotupatia Mungu wa mbinguni, tumshukuru Mungu sana kwa Amani na utulivu aliotupa na tuendelee kumuomba ili atuepushe na kila aina ya dhahama na uharibifu wa Yule adui!
Kama tulivyosikia hivi karibuni, yale yaliyotokea nchi jirani ya Kenya, kwa hakika tunawapa pole sana kwa mkasa huo, pole kwa wale waliowapoteza wapendwa wao na wale waliojeruhika tunawaombea wapone haraka, tunaamini hekima ya Mungu itakuwa juu ya serikali yao kushughulikia jambo hilo kikamilifu.
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai, hata sasa tunapoende kumalizia robo ya tatu ya mwaka 2013, tumeshuhudia mambo mengi sana mwaka huu ya kila aina, yapo yale yalionza kwa mara ya kwanza na mengine yamekuwa ni mwendelezo tu wa yale yadumuyo au yalioyaanza hapo kale, tumeshuhudia michezo mbalimbali na vipaji lukuki vikiinuka na kuimarika katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, na kwa yote mema na mazuri tunampa Mungu Utukufu kwa hakika!


UTANGULIZI JUU YA JOHN LISU;

John Lisu ni mmoja wa waimbaji/Waabudishaji wanaoheshimika katika Tasnia ya muziki wa Injili kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kukuza na kuendeleza muziki wa Injili nchini Tanzania na nje ya Nchi. Nyimbo nyingi alizozitunga na kuziimba zimekuwa zikitumika katika makanisa mbalimbali kama nyimbo za kusifu na kuabudu; pia waimbaji wengine waliokua wakiimba naye wameweza kukua na kufikia uwezo wa kuwa waimbaji wa kujitegemea. John Lisu pia ametia hamasa kubwa miongoni wa wanamuziki wa Injili kuanza kufanya muziki wa live. John Lisu ameweza kufanya tours za ndani ya Tanzania, Africa na Bara la Ulaya kwa ajili ya huduma.
CHRISTINA SHUSHO

John Lisu anategemea kufanya Project II ya Live recoding inayojulikana kama "UKO HAPA" baada ya project ya kwanza ya Jehova yu hai kufanya vizuri sana. Tamasha litafanyika ndani ya ukumbi wa City Christian Centre (CCC) Upanga tarehe 6 Octoba 2013, kuanzia saa 8. mpaka saa 2 usiku.
PAUL CLEMENT

 Tamasha litasindikizwa na waimbaji nguli kama Christina Shusho, Neema Gospel Choir, Paul Clement, Pastor Safari Paul, Bomby Johnson Waimbaji wote wamethibitisha kuwepo. 

BOMBY JOHNSON

VENUE:
City Christian Centre (CCC) mkabala na chuo kikuu cha mzumbe
Si mbali saana kutoka Diamond Jubilee
MIRIUM LUKINDO WA MAUKI


USAFIRI (basi zilizobandikwa matangazo ya tamasha) utakuwepo kutoka posta mpya kwenda ukumbini kuanzia saa saba na nusu mchana kwa bei ya kawaida.
PASTOR SAFARI PAUL

HABARI NJEMA-MUHTSARI!!!!!

Sasa kwa mara pili nchini Tanzania, mwimbaji WA NYIMBO ZA INJILI na mwabuduji JOHN LISSU wa jijini Dar Es Salaam, atakuwa anafanya Ibaada kubwa ama Tamasha la kusifu la Kuabudu(LIVE PERFORMANCE), litakalorekodiwa moja kwa moja (DVD LIVE RECORDING) lenye jina “UKO HAPA” (Yaani Mungu na Uwepo wake).
Tamasha hilo litafanyika jumapili ya Tarehe 6, Octoba 2013  katika Ukumbi mkubwa wa kisasa wa Kanisa la City Christian Centre (CCC)- Upanga, mkabala na Chuo Kikuu Mzumbe – tawi la Dar es salaam, kuanzia saa nane mchana.
Tunataraji watu 5000 kuwa sehemu ya tamasha hili la kipekee,Utakuwa sehemu ya tamasha hilo kwa tiketi ya 10,000/= (kawaida), 20,000/= (VIP) na 3000/= (Watoto);
na Kwale watakaohitaji tisheti maalum za tukio hilo, basi zinapatikana kwa kati ya 12,000-15,000/=, wewe wasiliana tu na (0713905118)
NELLY-MKE WA JOHN LISU


VITUO VYA KUUZIA TIKETI;
1.   MWENGE – Tarakea duka la Kanda
2.   KINONDONI – DPC
3.   MLIMANICITY – Silverspoon Restaurant
4.   KARIAKOO – Mbogo Shop
5.   UKONGA BANANA – KWA GIDO
6.   POSTA - DUKA LA MSAMA

T-SHIRTS

-T-shirts maalumu kwa wanaume na wanawake zinapatikana katika vituo vya kuuzia tiketi kwa bei ya elfu kumi, mpaka elfu 15(kutegmeana na aina).

N.B; Kwa tiketi ya VIP, mnunuzi atajipatia na Audio CD ya John Lissu ya “Uko Hapa”

USAFIRI UTAKUWEPO!!
Siku ya tamasha kutakuwepo usafiri kutoka Posta Mpya mpaka CCC-Upanga,eneo la tukio, hivyo kama wewe ni mgeni na hupafahamu mahali hapo, basi utakachotakiwa kufanya ni kupanda magari toka ulipo mpaka posta mpya kabla ya saa nane,na hapo utayakuta mabasi yenye mabango ya Tamasha, basi utajongea humo na hapo utawezeshwa kufika eneo la tukio, muhimu ni kuzingatia muda!

MUHIMU SANA!!

JOHN LISU NA TIMU NZIMA WAKIWA MAZOEZINI


Tamasha hili ni muhimu sana kwa Tanzania, hasa ukizingatia JOHN LISSU ni mmoja wa waimbaji wa kwanza kuimba live kila mahali anapoalikwa na ni mwimbaji wa kwanza binafsi kufanya LIVE DVD RECORDING pale Ubungo plaza, na ile ya kwanza iliitwa “JEHOVA YU HAI” na sasa anafanya LIVE RECORDING kwa viwango vingine bora zaidi, maana Mungu hutupa hatua moja zaidi kila siku.
Ni muhimu kwa kila mtanzania kujivunia kipaji na tukio hili muhimu katika historia, njoo umwabudu na kumsifu Mungu pamoja, Njoo ujifunze, Njoo umuunge mkono mtanzania mwenzako na njoo uje ufanyike sehemu ya Historia hii kwa Utukufu wa Jehova.
NEEMA GOSPEL CHOIR-KWAYA PEKEE ITAKAYOSHIRIKI "UKO HAPA"


MWALIKO MAALUM;
Kipekee Ninapenda kuwakaribisha wachungaji, mitume, manabii, wainjilisti, waalimu na viongozi wote wa makanisa na huduma mbalimbali, ninawakaribisha viongozi wote wa kisiasa na kijamii kutoka serikalini na vyama vya siasa vyote, ninapenda kuwakaribisha wanaharakati na wanataaluma wote, ninapenda kuwakaribisha waimbaji wote wa nyimbo za injili na wanasanaa wote, ninapenda kuwakaribisa wanafamilia wote, asiwepo wa kubaki nyuma, ninapenda sasa kukukaribisha wewe unaesoma hapa, naam nisaidie kumkaribisha na mwenzako na yeye aje na mwenzake, kimsingi tukio hili ni letu wote bila kujali kitu chochote, njooni tumsifu na kumwabudu Bwana na Mungu hataacha kuibariki Tanzania!
EMMANUEL NDIYE ATAKAYEMPIGIA JOHN LISU LEADING GUITOR


SHUKRANI;
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Hakneel Production (Wadhamini wakuu), na Jonn Lissu na timu nzima ya maandalizi; Kanisa la CCC-Upanga; vyombo vya habari hususani Praise Power na WAPO Radio; Clouds TV kupitia CHOMOZA na Clouds Radio kupitia GT; Sibuka Tv kupita Gospel Hits; Bloggers hususani Christian Bloggers, magazeti na vyombo vingine vyote vya habari! Shukrani hizi zimfikie kila mtu mmoja mmoja aliyetoa mchango wa mawazo, fedha, ushauri, maombi, ubunifu, yaani mchango wowote wa hali na mali na Mungu awabariki nyote!
MIRIUM LUKINDO WA MAUKI


MUHTASARI MKUU;
Tukio; TAMASHA LA KUSIFU NA KUABUDU, LITAKALOREKODIWA
(DVD LIVE RECORDING CONCERT)
Mhusika; JOHN LISSU
Jina: “UKO HAPA”
Mahali; UKUMBI WA KANISA LA CITY CHRISTIAN CENTRE (CCC)- UPANGA
Lini; 06TH OCTOBA, 2013
Muda; KUANZIA SAA NANE MCHANA
Kiingilio; Tsh 10,000/= (kawaida); 20,000/= (VIP) na 5000/= (Watoto)

Wasindikizaji; CHRISTINA SHUSHO, MIRIUM LUKINDO, PASTOR SAFARI, BOMBY JOHNSON, NEEMA GOSPEL CHOIR-AIC Chang’ombe na PAUL CLEMENT.

Mengineyo; USAFIRI UTAKUWEPO TOKA POSTA MPAKA CCC-UPANGA na Unaweza kujipatia Tisheti pia.
Wahusika; WATU WOTE MNAKARIBISHWA!


UKIPATA HABARI HII USIACHE KUMSHIRIKISHA NA MWENZAKO, NAAMINI HAUTAKOSA TUKIO HILI MUHIMU LA KIHISTORIA KATIKA NCHI YA TANZANIA KWA UTUKUFU WA MUNGU!!

KWA PICHA NA TAARIFA ZAIDI;


http://www.youtube.com/watch?feature=player_detailpage&v=blz0PKQ6QNU
MAWASILIANO:
O713 240 397 – JOHN LISU
0713 905 118 –PROSPER MWAKITALIMA – EVENT MANAGER
0713 883 797 - FREDY CHAVALA - PUBLICITY


Imetolewa na;
Fredy E. Chavala <King Chavala (MC)>
Publicity Manager
+255 713 883 797
On Behalf of The Organizing Committee

Thursday, August 8, 2013

KITALU CHA MADINI CHA EKARI 9.8 KINAUZWA TANGA!!!

KUNA KITALU CHA KUCHIMBA MADINI YA DHAHABU KILICHOPIMWA NA KINA HATI YA SERIKALI!
PAMEFANYIWA UTAFITI NA PAMEPIMWA, UKIWA KAMA MTU BINAFSI AU KAMPUNI AMA TAASISI, BASI UNAKARIBISHWA KUNUNUA KITALU KIMOJA!

KITALU HIKI KINA UKUBWA WA EKARI 9.8

KITALU HIKI KINAUZWA 350M, KAMA UNAHITAJI NA KUPATA MAELEZO YA KINA ZAIDI, BASI TUWASILIANE KUPITIA 0713 883797

JIPATIE KIWANJA SAFI KABISA KIGAMBONI,DAR ES SALAAM!!!

JIPATIE VIWANJA KWA KUJENGA NYUMBA YA KUISHI AMA NYUMBA YA BIASHARA;

1. KIWANJA 20x54m KWA 3.5M (KARIBU SANA NA BARABARA)

2. KIWANJA 50x50m KWA 4.5M (KINAFAA SANA KWA MAKAZI)

N.B; VIWANJA VYOTE HIVI VIKO KM 20 TOKA FERRY!

KAMA UNAHITAJI TAFADHALI FANYA HIMA TUWASILIANE KUPITIA 0713 883 797

Tuesday, August 6, 2013

OKOA MAISHA YA WATOTO YATIMA HAWA...KWA KUCHANGIA CHAKULA!!

SHALOM!
HABARI ZENU WAPENDWA!!
NINAAMINI MNA MOYO WA UPENDO, TENA WA KUWAJALI WENGINE KULIKO NINYI, NA HATA ZAIDI BIBLIA INASEMA UPENDO WA KWELI NI ULE WA KUWAPENDA WENGINE ZAIDI.
*****HANANASIFU ORPHANAGE CENTRE (HOCET)....HAWANA CHAKULA KABISAAAAA NA WEWE NA MIMI PEKEE NDIO TUNAWEZA KUWALISHA KWA SIKU 120, KABLA HAWAJAANZA KUJITEGEMEA****
LEO NINALO OMBI MAALUM KWENU, NI MUHIMU SANA SANA....KUNA KITUO KIMOJA CHA KULELEA WATOTO YATIMA (WATOTO WA MUNGU), KITUO KINACHOENDESHWA NA WATU TU WALIOJITOLEA, NA HAPO AWALI KILIKUWAQ KINAFADHILIWA NA WAZUNGU FULANI, LAKINI BAADA YA KUONA WATOTO HAO WAMEKAZANA NA MUNGU NA HAO WAZUNGU (WAFADHILI) WAKAWEKA MASHARTI, ETI KAMA WAKITAKA WAENDELEE KUPOKEA MISAADA YAO BASI WAACHANE NA HAYO MAMBO YA YESU YESU....NA KWA KUWA HAKUNA BABA MWINGINE ZAIDI YA MBINGUNI NA HAKUNA  NAMNA BINADAMU ANAWEZA KUISHI KWA MISAADA YA BINADAMU MWINGINE BAADA YA KUMKANA MUNGU WA KWELI.
 
SASA WATOTO HAO WAKO KWENYE ENEO LAO LA SHULE WANASOMA NA WANAYO MIRADI AMBAYO BADO HAIJAANZA KULETA FAIDA ILI WAWEZE KUJIENDESHA WENYEWE, NAHIYO ITAKUWA HIVYO TU BAADA YA MIEZI MITATU AU MINNE KUANZAIA SASA.
WATOTO HAWA KWA SASA HAWANA CHAKULA KABISA, NA HATA LEO WAMEKULA KWA MSAADA WA KIJANA MMOJA ALIJITOLEA YEYE BINAFSI NA FAMILIA YAKE....MBALI NA GHARAMA NYINGINE ZA UENDESHAJI KAMA MISHAHARA/POSHO ZA WALIMU;
************************************************************************************************
KITUO HIKI KINATUMIA UNGA KILO 30, MAHARAGE KILO 14 NA SUKARI KILO 5....NA IKIWA NI WALI,BASI HUHITAJIKA KILO 30 ZA MCHELE KWA MLO MMOJA....NA PIA UNAWEZA KUCHANGIA MAFUTA NA FEDHA KWA AJILI YA VITU VINGINE VINAVYOWEZA KUHITAJIKA.
************************************************************************************************
NINAAMINI KWA MSAADA WA WATANZANIA WOTE WENYE MAPENZI MEMA NA WATOTO WA KITANZANIA, WATOTO HAWA HAWATAKOSA CHAKULA KWA SIKU HIZI 120 ZA MPITO KABLA HAWAJAANZA KUJITEGEMEA WENYEWE, SIO LAZIMA ULETE MSAADA MKUBWA SANA, LAKINI NAAMINI UNAWEZA UKAJITOLEA CHAKULA KIASI JAPO KWA SIKU MOJA TU KAMA SIO TATU, YAWEZA KUWA WEWE BINAFSI AU KAMPUNI AU FAMILIA AU KANISA, LAKINI NINACHOKIAMINI NI KUWA KAMA KWELI TUNAAMINISHA KUMPENDA MUNGU NA KUWAPENDA WATOTO WATANZANIA TENA WANAOLELEWA KATIKA MALEZI YA KIMUNGU BASI LAZIMA WATOTO HAWA WATAISHI BILA HOFU YA CHAKULA KWA SIMU HIZI 120, NA KWA HAKIKA BWANA ATAKUBARIKI SAWASAWA NA IMANI YAKO KWAKE
YAK 1:27 "....DINI ILIYO SAFI ISIYO NA TAKA MBELE ZA MUNGUBABA NI HII, KUWATAZAMA WAJANE NA YATIMA KATIKA DHIKI YAO NA KUJILINDA NA DUNIA PASIPO NA MAWAA"
MSAADA HUO UNAHITAJIKA SANA SANA, NAAM KWA NAMNA YOYOTE ILE UNAYOWEZA KUCHANGIA BASI USISITE,FANYA HIVYO...SADAKA YAKO YA KUWALISHA WATOTO HAWA HAITASAHAULIKA HATA KIDOGO, UNAWEZA KULETA MCHANGO WAKO WA CHAKULA PALE OFISI ZA NIIM COMPUTERS, MOROCO HOTEL AU UKATUMA MCHANGO WAKO WA FEDHA KWA NJIA YA SIMU, NAAM KWA MAULIZO ZAIDI 
TAFADHALI WASILIANA NA WASIMAMIZI NA WARATIBU WA ZOEZI HILI KWA NO.
0713 26 1425 na 0754 527955, pia 0783 757051
KWA NIABA YA WASIMAMIZI WA KITUO HIKI NINAWASHUKURU HATA KABLA HAMJAFANYA JAMBO LOLOTE MAANA NAAMINI UMEGUSWA NA UKO TAYARI SASA KUWASAIDIA WATOTO HAWA...KAMA TUNAWEZA KUCHANGIA SHEREHE ZA HARUSI, NAFIKIRI HATMA YA WATOTO HAWA NI ZAIDI,MUNGU AKUBARIKI UNAPOMSHIRIKISHA NA MWENZAKO!!
 
Imeandikwa na
KING CHAVALA MC
KWA UDHAMINI MKUBWA WA CHAVALA IDEAS PLATFORM.

Monday, August 5, 2013

NOTHING CALLED "TIME MANAGEMENT" IN REALITY!!!

Hello Entrepneurs, what's up?
Hope you are doing fine and you are still thriving to make better life by this one and that one.

I am sure you have attended several seminars, workshops and others of that kind and perhaps you have come across words like "PRINCIPLES OF SUCCESS"; "PRIORITIZE YOUR EFFORTS" AND "TIME MANAGEMENT".....ETC.

But personally i have gained interest on this one "TIME MANAGEMENT"

I have been pondering and meditating the detail of this statement and finaly i came to realize that there is Nothing like that in Reality.WHAT IS TIME?

Time is a dimension in which events can be ordered from the past through the present into the future, and also the measure of durations of events and the intervals between them. Time has long been a major subject of study in religion, philosophy, and science, but defining it in a manner applicable to all fields without circularity has consistently eluded scholars.Nevertheless, diverse fields such as business, industry, sports, the sciences, and the performing arts all incorporate some notion of time into their respective measuring systems. Some simple, relatively uncontroversial definitions of time include "time is what clocks measure" and "time is what keeps everything from happening at once".
Two contrasting viewpoints on time divide many prominent philosophers. One view is that time is part of the fundamental structure of the universe — a dimension independent of events, in which events occur in sequence. Sir Isaac Newton subscribed to this realist view, and hence it is sometimes referred to as Newtonian time.The opposing view is that time does not refer to any kind of "container" that events and objects "move through", nor to any entity that "flows", but that it is instead part of a fundamental intellectual structure (together with space and number) within which humans sequence and compare events. This second view, in the tradition of Gottfried Leibniz and Immanuel Kant, holds that time is neither an event nor a thing, and thus is not itself measurable nor can it be travelled.
Time is one of the seven fundamental physical quantities in the International System of Units. Time is used to define other quantities — such as velocity — so defining time in terms of such quantities would result in circularity of definition.An operational definition of time, wherein one says that observing a certain number of repetitions of one or another standard cyclical event (such as the passage of a free-swinging pendulum) constitutes one standard unit such as the second, is highly useful in the conduct of both advanced experiments and everyday affairs of life. The operational definition leaves aside the question whether there is something called time, apart from the counting activity just mentioned, that flows and that can be measured. Investigations of a single continuum called spacetime bring questions about space into questions about time, questions that have their roots in the works of early students of natural philosophy.
Furthermore, it may be that there is a subjective component to time, but whether or not time itself is "felt", as a sensation or an experience, has never been settled.
Temporal measurement has occupied scientists and technologists, and was a prime motivation in navigation and astronomy. Periodic events and periodic motion have long served as standards for units of time. Examples include the apparent motion of the sun across the sky, the phases of the moon, the swing of a pendulum, and the beat of a heart. Currently, the international unit of time, the second, is defined in terms of radiation emitted by caesium atoms (see below). Time is also of significant social importance, having economic value ("time is money") as well as personal value, due to an awareness of the limited time in each day and in human life spans.

WHAT IS MANAGEMENT? 

Management in all business and organizational activities is the act of coordinating the efforts of people to accomplish desired goals and objectives using available resources efficiently and effectively. Management comprises planning, organizing, staffing, leading or directing, and controlling an organization (a group of one or more people or entities) or effort for the purpose of accomplishing a goal. Resourcing encompasses the deployment and manipulation of human resources, financial resources, technological resources, and natural resources.
Since organizations can be viewed as systems, management can also be defined as human action, including design, to facilitate the production of useful outcomes from a system. This view opens the opportunity to 'manage' oneself, a prerequisite to attempting to manage others.

For that reason SOMEONE CAN ONLY MANAGE HIS/HER ACTIVITIES IN ORDER TO BE IN TIME!!

SO LET IT BE KNOWN THAT, NO ONE CAN HAVE CONTROL OVER TIME BUT YOU CAN HAVE CONTROL OVER YOUR ACTIVITIES!! 

PHORNESIS WEAR....SPECIALIZED IN DESIGNING,FASHION,PRINTING AND MODELING!!

OFFICIAL WEARING SPONSORS OF KING CHAVALA MC!!!

THERE ARE VARIETY OF DESIGNINGS....JUST YOUR CHOICE!!!
GET EXECUTIVE SUITS, CASUAL SUITS, PROFFESSIONAL WEARS FOR PEOPLE SUCH AS PASTORS,LAWYERS.JUDGES,DOCTORS,DRIVERS,SCHOOL UNIFORMS,GRADUATION GOWNS AND MANY OTHER PROFFESSIONALS PER YOUR ORDER!!!

WE ARE DOING DESIGNING FOR ARTISTS AND DIFFERENT PERFOMERS, WEDDINGS AND FOR OTHER EVENTS!!

WE ARE DOING MAKERTING AND MODELLING FOR DIFFERENT OTHER DESIGNERS!!

PHORNESIS WEAR....Smartness is Wisdom!!

Hotline +255 713 883 797

Sunday, August 4, 2013

KWANINI NINAMKUBALI SANA DR.REGINALD MENGI!!

inaendelea.....
NINAAMINI NINA MENGI YA KUSHARE NA DK.MENGI....NAAM NINA MENGI YA KUSHARE NA NINYI KUHUSU MENGI,LAKINI  NINAAMINI TUTAFAIDIKA WOTE KATIKA HILI...KAKA NA RAFIKI YANGU ERIC SHIGONGO NI MMOJA WA WATU AMBAO WANAMTAZAMA SANA DK MENGI KAMA DIRA NA ERIC ANATAMANI SANA SIKU MOJA AMPITE KABISA MENGI NA HII NI KWASABABU AMEPEWA MWANGA NA KUHUSIWA MENGI NA DK MENGI natamaniVIJANA WA KITANZANIA TUJIFUNZE TOKA KWA WAZEE WETU,NAAM WALE WALIOKULIA KATIKA MAZINGIRA YETU NA SIO KUSOMA TU HABARI ZA KINA BILL GATES NA KYOSAKI WA MBALI HUKO AMBAO HATA MAZINGIRA YA MAISHA YAO HAYAFANANI NA SISI!!!

MENGI ANASEMA..."UKITAKA FEDHA/MSAADA LAZIMA UWE NA WORKABLE IDEA KWANZA AMBAYO UNAYO HAKIKA KUWA INA MANUFAA NA HIYO ITADHIBITIKA TU KAMA UMESHAANZA KUFANYIA KAZI IDEA HIYO,HATA KAMA NI KWA KIWANGO CHA CHINI"

 ...USITAMANI TU KUOMBA HELA KILA WAKATI NA SIO KILA AKUNYIMAE HANA ILA HAONI FAIDA YA KUKUHARIBU KWA KUKUPA KITU USICHOJUA KUKIHANGAIKIA MWENYEWE...."OMBA NYAVU-UFUNDISHWE KUVUA,SIO KUOMBA SAMAKI NA BADO UNAAZIMA PA KUKAANG'IANITAENDELEA TENA WAKATI MWINGINE KUKUJUZA KWANINI HASA  NINAMUHESHIMU NA KUMKUBALI MFANYABIASHARA HUYU WA KICHAGA!!

......TO BE CONTINUED!!!

Wednesday, July 24, 2013

USHINDANI WA BIASHARA NDIO UKO HIVI??

KAMA UKIYAANGALIA VEMA UTAGUNDUA KUWA TIGO WAMEWEKA BANGO LAO JUU YA MABANGO YA VODACOM, TUNAJUA KUWA HAWA NI WASHINDANI LAKINI HIVI INARUHUSIWA????

Wednesday, July 17, 2013

.....EVERY BUSINESSMAN AND ENTREPRENEUR AT ANY CAPACITY MUST ATTEND THIS SEMINAR WITH AZIM JAMAL!!!

KWANINI....NAMKUBALI SANA NA KUHESHIMU MNO DR.REGINALD MENGI(01)!!!

NAAMINI WEWE NI MZIMA NA UNA NGUVU TELE,NA HILO NINALIAMINI KWASABABU UNGEKUWA HUJIWEZI USINGEJITAABISHA KUPEKUA MITANDAONI KUNA NINI!!
KIMSINGI NAOMBA NICHUKUE FURSA HII KUKUSALIMIA KIPEKEE WEWE UNAYESOMA HAPA NA NAAMINI UNAJITAMBUA NA UNA NDOTO AMBAZO UNGETAMANI KUZIFIKIA.....HONGERA KAMA UMESHAANZA KUTEKELEZA NDOTO HIZO HATA KAMA NI KWA KIWANGO KIDOGO!!

LEO NIMETAMANI NIWAKILISHE HAYA YALIYO MOYONI MWANGU,NAAM NI HAYA KUMHUSU MZEE WANGU NA RAFIKI WA UKWELI,DR.REGINALD MENGI!

MIMI BINAFSI SIWEZI KUJISIFU KUWA ETI NINAMFAHAMU SAAAANA LAKINI KIMSINGI NINAMFAHAMU,NA NILIKUWA NINAMFAHAMU KWA KUMSIKIA NA KUMWONA KWENYE TV TANGU ZAMANI KABLA YA SIJAHUDHURIA MATUKIO AMBAYO AMEKUWA AKIALIKWA KAMA MGENI RASMI,KAMA MZUNGUMZAJI,KAMA MJASIRIAMALI AU HATA KAMA MZEE WA HESHIMA KATIKA JAMII.....NA NILIMFAHAMU ZAIDI NILIPOKUTANA NAE NA KUZUNGUMZA NAE MAMBO MAWILI MATATU KAMA MARA TATU HIVI KATIKA MAENEO TOFAUTI TOFAUTI, NA NINA AMINI KUNA WAKATI NITAPATA MUDA MREFU ZAIDI WA KUKAA NA KUZUNGUMZA NA YEYE WA KUPATA HEKIMA ZAKE KAMA BABA NA MTANGULIZI ANAYEJUA MENGI HUSUSANI YALE NINAYOYAENDEA, NAAM IPO SIKU NITAMTOA LUNCH AMA DINNER NA NAAMINI NITAPATA MENGI HAHAHAHAH!

NIMEJITAHIDI KUSOMA NA KUSIKILIZA SANA WATU WANASEMA NINI JUU YAKE NA YAPI YANAYOTOKEA KUMHUSU....NIMEKUWA NIKIFUATILIA SANA MAISHA YAKE,JINSI ANAVYOISHI NA NAMNA ANAVYOJITOA KWA JAMII YAKE....KUSEMA KWELI MTAZAMO WANGU ULIBADILIKA KABISA SIKU NILIPOMSIKIA AKIFANYA PRESENTATION FULANI YA KUWASAIDIA WANAFUNZI!

JAMBO LA KWANZA;
NILIPENDA SANA KWA JINSI ALIVYOJISHUSHA NA KUAMUA KUJA KUONGEA NA WANAFUNZI WA CHUO BILA KUMLIPA WALA BILA NYODO NA ZAIDI AKAJITOLEA KUWASAIDIA WANAFUNZI HAO KUENDESHA SHUGHULI YAO....(HIYO ILIKUWA ISWIT 2009)
HII SIO RAHISI SANA KWA WATU WENGI WALIOFANIKIWA,KUMPATA TU NI ISSUE SEMBUSE KUMLETA AJE ASEME NA WANAFUNZI!....BASI DK MENGI NIKAONA NI MTU WA TOFAUTI SANA,MNYENYEKEVU NA ALIYEJISHUSHA.

JAMBO LA PILI;

NI MTU ANAESIKILIZA SANA,TENA KWA UMAKINI...NA HII INATEGEMEANA SANA NA KILE UNACHOWASILIANA NAE KWA SAA HIYO....KWA MFANO MIMI NILIONGEA NAE MARA YA KWANZA KWA UKARIBU SANA 2009 LAKINI HATA TULIPOONANA 2012 NA KUENDELEA AMEENDELEA KUNIKUMBUKA,NA KILICHONISHANGAZA NI KUONA KUWA HATA JINA HAJALISAHAU HALI MIMI NI MTU TU HUKU CHINI HAHAHAH! (SIJUI LABDA KWASABABU MIMI NI COMEDIAN LABDA)
....LAKINI KWA HILI LA KUSIKILIZA NINAMPONGEZA SANA,SHIDA YETU MOJA NI HII...WATU WENGI TUNAPOKUTANA NA WATU WENYE FEDHA AU WALIOFANIKIWA CHA KWANZA HUWA KINAKUWA NI KUOMBA FEDHA AU MSAADA FULANI,NA HILO NI KOSA KUBWA SANA NA NDIO MAANA WENGI HUFUNGA VIOO WASISIKILIZE MTU YEYETE NA HII INAWWATHIRI HATA WALE WALIO SERIOUS!

JAMBO LA TATU;
JAMBO LA TATU....NILIPENDA SANA ALIVYOFANYA PRESENTATION YAKE NA NAAMINI NDIVYO HIVYO HUWA ANAFANYA NA SEHEMU NYINGINE NYINGI....KWANZA ALIANZA KWA KUELEZA UHALISIA WA MAISHA YAKE TANGU ANAKUA HUKO KILIMANJARO,ALISEMA JINSI ALIVYOKUWA AKISOMA NA KULALA BANDANI AU JIKONI WAKATI MWINGINE NA ANAJUA KWENDA SHULE VILA VIATU....NA AKAELEZA JINSI ALIVYOANZA BIASHARA MDOGO MDOGO MPAKA HAPA ALIPO.....SIKU HIYO ALIWASILISHA KWA UTULIVU,KWA MIFANO HALISI NA KWA KUTUMIA NYIMBO ZA BAADHI YA WANAMUZIKI WAKONGWE DUNIANI.......NAKUMBUKA KUNA WAKATI ALIISIFIA SANA SAA YAKE YA MKONONI NA KISHA AKAWAITA WATU MBELE NA AKAWAAMBIA WATAZAME KWA MAKINI NA WAAMBIE WATU WENGINE ILE ILIKUWA NI SAA YA AINA GANI AU YA LABEL GANI?.......BASI WATU WALE WALIKAZANA NA WOTE WAKADHANI WAMEFAULU NA BAADA TU YA KUMALIZA AKAWAULIZA MLIPOKUWA MNACHUNGUZA MMEONA SAA INAONYESHA NII SAA NGAPI???/.....DAH HAKUNA HATA MMOJA ALIJIBU....NAAM NA SOMO LIKAWA KWANINI UNATAZAMA LAKINI HAUONI.....NA HAPO TUKAPATA SOMO KUWA IMETUPASA KUJIFUNZA KUONA KATIKA KUTAZAMA KWETU.
ALIONGEA VITU VINGI SANA AKASISITIZA SANAMTU KUWA NA NDOTO.....MTU KUWA NA MAONO.....MTU KUWA NA IDEA NA UANZE KUIFANYIA KAZI NA UNAPOMSHIRIKISHA MTU AU WATU BASI LAZIMA UWE UMEFIKA MAHALI FULANI PANAPOELEWEKA NA NDIO USAIDIWE KAMA INAHITAJIKA NA KUWEZEKANA HIVYO....SIO UNAWAZA TU JAMBO THEN MBIO KUOMBA MSAADA,HAPANA MAISHA HAYENDI HIVYO.
LAKINI PIA ALISISITIZA KUWA LAZIMA UJIAMINI NA KUAMINI KUWA UTAFANIKIWA TU.....NA HAPO ALICHEZA ULE WIMBO UIMBWAO..."I BELIEVE I CAN FLY"  NA HIYO IMEFANYA WIMBO NISISAHAU HATA KIDOGO NA KILA NINAPOUSIKIA HUWA NINAKUMBUKA PRESENTATION YA DR.MENGI SIKU ILE.   KWA HAKIKA ILIKUWA NZURI SANA NA NILIMFURAHIA SANA MAANA SIKUTEGEMEA KAMA ANGEWEZA KUWASILISHA KWA KIWANGO CHA KUELEWEKA NAMNA ILE!!

BAADA YA YEYE KUMALIZA NILIPATA BAHATI YA KUZUNGUMZA NAE NA APPROACH YANGU ILIMFANYA ANITAZAME KWA MAKINI SANA....NILISEMA..."SHIKAMOO BABA,POLE NA MAJUKUMU NA HONGERA KWA NICE PRESENTATION.....MIMI NAITWA CHAVALA NA NI MWAJIRI MWENZIO,NINATAMANI SIKU MOJA NIKUONE ILI UNISAIDIE KWA KINA NI JINSI GANI UMEEDELEA KUSTAWI KATIKA BIASHARA HATA LEO" BASI AKASEMA "THAT IS VERY GOOD" AKANIPA BUSINESS CARD NA TUKAACHANA.....BUT THAT WAS FIRST TIME AND FOUNDATION OF OUR FRIENDSHIP!!

WENGI WAMEKUWA NA YAO YA KUSEMA JUU YA MZEE HUYU,NA MENGINE YAMEKUWA NA SURA YA UGOMVI WA KIBIASHARA NA WENGINE WAMEJIKUTA WAKIMTUKANA BILA SABABU,LAKINI JUU YA YOTE NA MADHAIFU YOYOTE YALE ALIYO NAYO,HESHIMA YAKE NA MCHANGO WAKE KWA JAMII HII YA WATANZANIA LAZIMA UHESHIMIWE....LAZIMA TUKUBALI KUWA KWA VYOMBO VYAKE VYA HABARI NA MAKAMPUNI YAKE...KUNA WATU WENGI SANA WAMEFAIDIKA NA FAMILIA ZAO.....NAWAFURAHIA SANA WATU WANAO-APPRECIATE WENGINE NA SIO WA KUPONDA TU KILA SIKU!!

Dk Mengi na Constatine

                                        .......TO BE CONTINUED!!!!!

 

NA KING CHAVALA
(MC/STAND UP COMEDIAN)
Business & Mgt Consultant
+255 713 883 797

Friday, July 5, 2013

BUSINESS IS ALL ABOUT CONVICTION AND NEGOTIATION!!!

Hello my friends and Businessmen!
I am talking to Entrepneurs!
Many people fail in business because they lack informations and deep insight!
You can decide to trade whatever worth to humanbeings!!!
Here is an example of how business can be defined;

What is BUSINESS ?

Dad: I want u 2 marry a girl of my choice.
Son: No
Dad: The girl is Bill Gate’s daughter.
Son: then Ok.

Dad goes to Bill Gates.
Dad: I want your daughter to marry my son.
Bill Gates: No
Dad: My son is the CEO of the World Bank.
Bill Gates: Than ok

Dad goes 2 the President of the World Bank.
Dad:Appoint my son as the CEO of your bank.
President:No
Dad:He is the son-in-law of Bill Gates.
President: Then OK

That’s business…!!


SO ONCE A DAD MEET ALL OF HIS REQUIREMENTS TIMELY,THEN THAT IS BUSINESS!!

Thursday, June 20, 2013

KWA KAZI ZOTE ZA PRINTING "MGAYA INVESTIMENT!!!",WAKO KWA AJILI YAKO!!!

HABARI NJEMA KWA WAJASIRIAMALI NA WASHIKA DAU WENGINE WOTE!
 KWA MAHITAJI YAKO YOTE YA PRINTING BASI UMEPATA JIBU!!!
>>HUSUSANI T-SHRT ZENYE MAANDISHI MBALIMBALI YENYE MAADILI!

MGAYA INVESTIMENT WANAOPATIKANA MAENEO YA UBUNGO NYUMA YA UBUNGO PLAZA WANAFANYA PRINTING ZA T-SHRTS(kwa ajili ya sherehe,misiba na matumizi ya kawaida);WHEEL COVERS,CALENDERS AND MANY MORE!!!
HUNA HAJA YA KUHANGAIKA,HEBU JIUNGE NA WAJASIRIAMALI WENZAKO KWA KUUNGA MKONO KAZI ZAO!!
For promotion!!

For T-shrt

For wheelcover

KAZI ZINAFANYIKA HARAKA,KWA UBORA NA UMAKINI KWA BEI NZURI MNO AMBAYO HUJAWAHI IPATA POPOTE!!!
BASI TUPIGIE SIMU SASA NASI TUTAKUHUDUMIA UPENDAVYO;
+255 712 611 614
KARIBUNI SANA!!

IMETOLEWA NA MKURUGENZI MKUU
STEPHEN MGAYA

@IMETOLEWA KWA UDHAMINI WA MJASIRIAMALI+ BLOG 
Hotline<+255 713 883 797>

"The PRINCIPLE of GROWTH"....GET YOUR COPY NOW!!!

THIS IS VERY GOOD BOOK FOR ANYBODY TO READ AND GROW BY SHEMEJI MELAYEKI ADAM!!!
JUST CALL +255 714 548 565

@KWA HISANI KUBWA YA MJASIRIAMALI+ Blog

HOTLINE +255 713 883 797

ONYO: EWE MJASIRIAMALI JIHADHARI NA UTAPELI HUU!!!!

UKIPATA TAARIFA HII,MJULISHE NA MWENZAKO!!!
NA +255 713 883 797

Saturday, March 9, 2013

HILI NI ZAIDI YA SHAIRI KWAKO MJASIRIAMALI!!

From Malenga wa Mvita by Ahmad Nassir
UJANA
            

                    1
           Ewe ulo na busara, fikiri bibi na bwana,
           Fikiri lilo tohara, na lile lilo dhamana,
           Pia fikiri izara, wewe nayo kukutana,
           Sihadawe na ujana, na ujana una mwisho

                    2
           Ujana ni jambo bora, ameupamba Rabana, 
           Tena umetia fora, ulitendalo hufana,
           Basi usiwe mkora, akiba uweke sana,
           Sihadawe na ujana na ujana una mwisho.

                    3
           Kuweka jambo dharura, jihimu kuweka mwana,
           Siyo pato kulipura, kwa usiku na mchana,
           Ukitoweka ujura, elewa umekubana,
           Sihadawe na ujana, na ujana una mwisho.
          
                    4
           Hebu zituze fikara, ushike ninayonena, 
           Akiba kwako sitam, ukiijaza shehena,
           Na pia huwa kafara, na shida isije tena,
           Sihadawe na ujana, na ujana una mwisho.
          
                    5
           Ufanyapo biashara, ewe kijana kazana, 
           Ujihimu kila mara, na akiba kushikana,
           Uzee ukikudara, uwe umetulizana,
           Sihadawe na ujana, na ujana una mwisho.
           
                    6
           Kwa kweli Si masihara, mwanadamu hutatana,
           Kukosa kitu ni dhara, jina hutojulikana,
           Au uitwe fukara, mzee mja wa lana,
           Sihadawe na ujana, na ujana una mwisho.
           
                     7
           Ujana hukuzingira, ukangiwa na fitina,
           Ukafikwa na majira, uzee ukawa jina,
           Basi na wako ujira. wa kazi weka hazina,
           Sihadawe na ujana, na ujana una mwisho
 
AKIWA KAMA MSHAIRI ANAWEZA KUWATIA MOYO WENGINE,LAKINI PIA HII NI FURSA PEKEE 
KWAKE KUISHI KWAYO MAANA HATA KIPAJI NI MSINGI WA BIASHARA NA MATUNDA YA KIPAJI
 NDIO BIDHAA YENYEWE YA KUWAUUZIA WATEJA WAKO!

Yako mengi tu huku http://www.mwambao.com/mashairi.htm

Monday, February 18, 2013

HALI HALISI KATIKA BIASHARA NI TOFAUTI NA KINACHOSEMWA NA WENGI KWENYE MAJUKWAA

KUNA HALI TOFAUTI KATKA BIASHARA NA KILE AMBACHO KINAFUNDISHWA JUKWAANI, WENGI WA WATU WANAOFUNDISHA WATU NAMAN YA KUFANYA BIASHARA UTAKUTA WENGI WAO HAWAJAWAHI KUUZA HATA NYANYA MBILI

MIMI NIMEANZA KUFANYA BIASHARA NIKIWA NA MIAKA 14 NIKIUZA UGORO, KUKU, MAJANI YA CHAI NA SUKARI NA NILIPOFIKISHA UMRI WA MIAKA 17 NIKAANZA KUTENGENEZA NA KUUZA SIME PAMOJA NA VISU.

NILICHOKIGUNDUA NI KWAMBA BIASHARA ZOTE ZINAZOKUWA ZINAHITAJI MOYO, KUTOKATA TAMAA, NA KUAMUA KUENDELEA HATA KAMA UNAPITA KATIKA KIPINDI KIGUMU......

NI VIZURI UKAWA RAFIKI NA BIASHARA YAKO, UIPENDE NA UIHUDUMIE...

NIMEGUNDUA MARA ZOTE NINAPOSHINDWA KUFANYA MAUZO NI KWA SABABU NILIKUWA SIZIKUBALI BIDHAA ZANGU.
NIKIWA NA MAWAZO HASI JUU YA BIDHAA ZANGU NASHINDWA KUFANYA MARKETING SAWASAWA. USHAWISHI KWA WATEJA UNAKUWA NI MDOGO.

NILIWAHI KWENDA KUUZA FULANA  KATIKA KANISA MOJA, LAKINI SIKU HIYO SIKUUZA HATA MOJA....NAKUMBUKA NILIPOTOKA NYUMBANI NILIKUWA NAZIONA KAMA HAZIJAPENDEZA VIZURI,
AHHH! KWA KWELI ZILINIPA TABU, KILA ALIYEPITA ALINIANGALIA SURA KISHA AKAPITA PEMBENI.. NILIRUDI NYUMBANI NIKIWA NA HASIRA ZA KUTOSHA,,,
 NILIPOGUNDUA HILI KUWA TATIZO LILIKUWA NI MIMI NA SIO BIDHAA ZANGU NIKAPANGA KURUDI TENA KANISA LILE,,,

SIKU HIYO NILIJIANDAA VIZURI SANA, NILIKUWA SMART, NIMEGONGA MY BEST PERFUME, MY BEST SHIRT NA TABASAMU LANGU NENE.

DAAAAH! KILA MTU ALIYEPITA ALICHUKUA FULANA, HATA WASIOKUWA NA HELA WAKAKOPA WENZAO. NILISHANGAA SANA

LOVE YOUR PRODUCTS, DON'T LOOK DOWN AT YOUR PRODUCTS, DON'T LOOK DOWN AT YOUR SELLING METHODS,,.....
YOU CAN SELL ANYTHING, ANYTHING , ANYTHING , ANYTHING , ANYTHING , ANYTHING , ANYTHING, ANYTHING , ANYTHING....ONLY WHEN YOU CHOOSE TO VALUE YOUR PRODUCTS


Sunday, February 17, 2013

NINI HASA MAANA YA UJASIRIMALI?

NAJUA UMESIKIA MARA NYINGI NA TAFSIRI NYINGI SANA KUHUSU UJASIRIAMALI!

YAMKINI UNAWEZA KUWA NA MAANA SAHIHI AU MAANA DHAIFU!!

LAKINI SASA HAPA NATAMANI UTOE MAONI YAKO HASA JUU YA MAANA UNAYOIFAHAMU WEWE KUHUSU UJASIRIAMALI NA HAPO MWISHONI TUTAONA TAFSIRI IPI INATUFAA KATIKA UHALISIA NA MATUMIZI RAHISI KATIKA MAISHA YETU!!

KARIBU UTOE MAONI YAKO!!!!

Monday, February 4, 2013

JIHADHARI MJASIRIAMALI#.....UTAPELI MPYA UMEINGIA MJINI!!

WAELEWE MATAPELI WALIOKUBUHU HAPA DSM....IMENITOKEA MM LEO 02/02/2013 KWA
MARA YA PILI


Kuna utapeli fulani unaendelea Tanzania na inaelekea wanaoufanya wamefanikiwa

sana na wanaendelea kufanikiwa kwani ni wa muda mrefu sasa. Nadhani matapeli

hawa wanatumia ujinga wetu maana sisi sio watu wakutafuta sana usahihi wa mambo

kabla ya kusema au kutoa maamuzi, pamoja na ujinga wetu wa kutaka kufanikiwa kwa

haraka kwa njia yeyote ile hata kama hatujafanya kazi na bila kutumia akili. Utapeli huu

sio mwingine bali ni ule wa wale watu wanaompigia mtu simu wakijifanya wanakujua

kabisa na wanaweza hata kukupa some backgrounds zako za kazi, ajira au elimu

na meninge hadi ukashawishika kuwa unayeongea naye ni mtu unayemfahamu/

munayefahamiana na hivyo kutokua na hofu na uhalisia wa anachokuambia. Baada ya

hapo wanaanza kukushawishi juu ya kuwasaidia kupata madawa ya kuhifadhi nafaka

kwa madai kuwa mawakala wao ambo wamekua wakizipata toka kwao wameanza

kuleta uswahili hivyo kwa vile unayeongea naye ndio anahusika na suppy, basi ameona

ni vema akutumie wewe “mpendwa anayekujua” ili angalau upate hiyo commission

kubwa ambayo huwapa ho mawakala na mugawane kidogo. Mara nyingi wanasema

wanafanya kazi na shirika la chakula duniani (FAO) au shirika la wakimbizi duniani

(UNHCR) na wako Kigoma.

Zaidi ya mwaka mmoja sasa nikiwa ofisini walinipigia na aliyekua anaongea name

alianza kwa kujitambulisha kama graduate wa kitivo cha uhandishi cha chuo Kikuu

Mlimani na kwamba tulisoma wote mwaka mmoja wakati nikisoma degree ya kwanza

lakini huenda simkumbuki kwa sababu nilikua kiongozi wa fellowship na siwezi kuwa

nakumbuka wote niliokua nawaongoza. Yeye alikua fellowship. Alikua akiongea kwa

kicheko na “bwana yesu” asifiwe nyingi ili kunionesha ni kwa kiasi gani namfahamu

na tunafahamiana. Kwa bahati mbaya wakati ananipigia nilishasikia kwa umbali juu

ya utapeli huo ambao kwa kipindi hicho ndio ulikua umeanza tu na kushika kasi huku

watu wengi wakiwa wamepoteza mamilioni. Hivyo alipoanza kuongea ujinga wake wa

kunipa commission and all that, nilimwambia tu kuwa sina muda wa kujihusisha na

biashara aliyokua “anataka kunisaidia ili nipate pesa za bure”, kwa haraka na bila jasho.

Alikua disappointed sana kwa jibu langu hasa kutokana na muda mrefu alioutumia

kunishawishi nikubali “msaada aliokua ananipa kama mpendwa mwenzake”.

Leo asubuhi majira ya saa nne nilipokea simu kwenye line yangu ya tigo na number

iliyonigia ni 0717-093260. Mtu aliyenipigia alikua anaongea kwa uchangamfu mkubwa

na kwa furaha huku akitaja majina yangu yote na kuniuliza iwapo kwa sasa niko DSM

au nimesafiri. Aliniambia kuwa kafurahi kusikia kuwa niko DSM kwani ndipo zilipo ofisi

zao na kwamba alitaka kuniunganisha zao ili nikachukue mzigo ambao utakua na cha

juu kizuri sana. Nilipoona anaendelea nilimuomba ajitambulishe...akaniambia anaitwa

Lameck na kuwa alishafanya kazi Planet International hapa chuo kikuu. Alipotamka

hivyo nikaanza kupata ukakasi kwani hapajawahi kuwa ofisi ya kampuni hiyo hapa

Mlimani. Nikamuuliza yuko wapi kwa sasa na kwa msisitizo akanijibu kuwa kwa sasa

yuko Serengeti National Park. Nikamuuliza iwapo anafanya kazi na TANAPA..akasema

hapana bali yuko na shirika moja la Kijerumani linalojishughulisha na wanyamapori...na

akijua kuwa niko Chuo Kikuu alitafuta style nzuri ya “kuniingiza alipokusudia” ...maana

alianza kunieleza kuwa shirika lao linafanya “tafiti za wanyama pori katika mbuga

yetu ya Taifa kubwa sana”. Bado nikiwa najaribu kuunganisha “idadi ya nukta kadhaa”

akaniona mjinga sana na kuanza kunielezea jinsi wanyawa walioko Serengeti wanavyo

migrate kila mwaka kwenda Kenya.....na kuwa wanahama wengi kama elfu mbili

hivi...(nikapata nukta nyingine)..then nikaingilia na kumsaidia kuwa hawavuki kwa

maelefu bali ni zaidi ya milioni moja wanahama na kurudi kila mwaka. Pomaja na utafiti

kazi nyingine wanayofanya ni pamoja na kutoa chanjo kwa wanyama hawa maana

wanaporudi wanakua wamerudi na magonjwa toka Kenya.

Hapa ndipo alipopotea njia zaidi kwani kati ya jambo ninalolijua kwa mapana

kidogo ni hii movement ya wild beasts, zebra na wengine walioko Serengeti .

Nikamuonesha kushangaa kuwa wanawezaje kuwapa chanjo

namna hii (na kumuonesha najua chanjo ni nini nikajifanya mhaya kidogo na kutamka

vaccination)...akaanza kujichanganya kuwa wao wana njia tatu za kutoa chanjo

maana ni kweli kuwa wanyama ni wengi...kwanza wanatengeneza majosho/mabwawa/

madimbwi ambayo wanaweka dawa na hiyo wale wanyama wanapokua wanarudi

wanatumbukia na hivyo automatically wanakua wamepata chanjo. Hapa akachemka

zaidi...nikamuuliza hivi kuogesha ng’ombe kwenye majosho ni chanjo au ni kuua

kupe na viroboto? Nikamuuliza kuna chanjo inafanyika juu ya ngozi?...alipoona hana

majibu akauma maneno mawili-matatu halafu akasema njia ya pili wanayotumia

ni kuwakamata wale wakubwa kama tembo na wengine na kuwapiga sindano za

chanjo....nikajizuia kucheka. Alipoona swali lingine linafuata kabla hajaanza kuningiza

kwenye “undani/details za deal” lenye commission ...akaomba udhuru kidogo kuwa

boss wao kaingia ofisini mara moja na hivyo atanipigia baadaye kidogo...akakata simu

na ukawa ndio mwisho wa mawasiliano

Alipokata simu tu nikamtext kuwa angeendelea tu na ujinga wake maana nawafahamu

vema na wanachokifanya...na huo ukawa ndio mwisho wa ile number kupatikana

hewani baada tu ya ujumbe wangu kuwa delivered.

Ushauri Kidogo:
• Unapojikuta kwenye mazingira ya mtu kujitambulisha kwako kwa nguvu kubwa huku

ukiwa humfahamu, mpe nafasi ya kuongea

• Unapojikuta kwenye mazingira ya kudanganyika kuwa unaweza kunufaika na kupa

utajiri kirahisi kwa mtindo wa ki_DECI_DECI au kimuujizaujiza, usichanganyikiwe

na kuanza kuutazama huo muujiza kama ndio umeshakufikia. Utafanya la muhimu

sana iwapo utaruhusu akili yako kufanya kazi na kutafakari vema kila unachokiona

au kukisikia

wanyama wengi

Kama unaweza, ni vema kurecord mazungumzo ambayo una wasiwasi nayo

• Kama unaweza, una nafasi, na una matumaini kuwa polisi wanaweza kuwa na

msaada kwenye hili, basi wasikilize watu hawa na kutafuta msaada wa polisi kwani

utaokoa na wengine wasidanganyike

• Tambua tu kuwa watu hawa wana mtandao mkubwa sana na mara nyingi

wanafanya mambo yao wakiwa na taarifa za kuwatosha na wamejipanga. Unaweza

ukawa kwenye mstari mwembamba sana unaotofautisha ukweli na uongo

• Kwa nini bado makampuni ya simu yanaruhusu simu kutumika ikiwa haijasajiliwa?

Na kama imesajiliwa, je wale wanaoandikisha hizi simu, wana ujuzi wowote wa

kugundua kitambulisho halali na ambacho ni fake watu wanavyovitumia kusajilia

simu zao?

Ufahamu na Akili tuliyonayo ukitumika vema bil haraka ya mafanikio tunaweza kukabiliana
na changamoto nyingi za kitapeli tunazokumbana nazo

IMEANDIKWA NA
MATHEW MNDEME a.k.a MM