Monday, February 18, 2013

HALI HALISI KATIKA BIASHARA NI TOFAUTI NA KINACHOSEMWA NA WENGI KWENYE MAJUKWAA

KUNA HALI TOFAUTI KATKA BIASHARA NA KILE AMBACHO KINAFUNDISHWA JUKWAANI, WENGI WA WATU WANAOFUNDISHA WATU NAMAN YA KUFANYA BIASHARA UTAKUTA WENGI WAO HAWAJAWAHI KUUZA HATA NYANYA MBILI

MIMI NIMEANZA KUFANYA BIASHARA NIKIWA NA MIAKA 14 NIKIUZA UGORO, KUKU, MAJANI YA CHAI NA SUKARI NA NILIPOFIKISHA UMRI WA MIAKA 17 NIKAANZA KUTENGENEZA NA KUUZA SIME PAMOJA NA VISU.

NILICHOKIGUNDUA NI KWAMBA BIASHARA ZOTE ZINAZOKUWA ZINAHITAJI MOYO, KUTOKATA TAMAA, NA KUAMUA KUENDELEA HATA KAMA UNAPITA KATIKA KIPINDI KIGUMU......

NI VIZURI UKAWA RAFIKI NA BIASHARA YAKO, UIPENDE NA UIHUDUMIE...

NIMEGUNDUA MARA ZOTE NINAPOSHINDWA KUFANYA MAUZO NI KWA SABABU NILIKUWA SIZIKUBALI BIDHAA ZANGU.
NIKIWA NA MAWAZO HASI JUU YA BIDHAA ZANGU NASHINDWA KUFANYA MARKETING SAWASAWA. USHAWISHI KWA WATEJA UNAKUWA NI MDOGO.

NILIWAHI KWENDA KUUZA FULANA  KATIKA KANISA MOJA, LAKINI SIKU HIYO SIKUUZA HATA MOJA....NAKUMBUKA NILIPOTOKA NYUMBANI NILIKUWA NAZIONA KAMA HAZIJAPENDEZA VIZURI,
AHHH! KWA KWELI ZILINIPA TABU, KILA ALIYEPITA ALINIANGALIA SURA KISHA AKAPITA PEMBENI.. NILIRUDI NYUMBANI NIKIWA NA HASIRA ZA KUTOSHA,,,
 NILIPOGUNDUA HILI KUWA TATIZO LILIKUWA NI MIMI NA SIO BIDHAA ZANGU NIKAPANGA KURUDI TENA KANISA LILE,,,

SIKU HIYO NILIJIANDAA VIZURI SANA, NILIKUWA SMART, NIMEGONGA MY BEST PERFUME, MY BEST SHIRT NA TABASAMU LANGU NENE.

DAAAAH! KILA MTU ALIYEPITA ALICHUKUA FULANA, HATA WASIOKUWA NA HELA WAKAKOPA WENZAO. NILISHANGAA SANA

LOVE YOUR PRODUCTS, DON'T LOOK DOWN AT YOUR PRODUCTS, DON'T LOOK DOWN AT YOUR SELLING METHODS,,.....
YOU CAN SELL ANYTHING, ANYTHING , ANYTHING , ANYTHING , ANYTHING , ANYTHING , ANYTHING, ANYTHING , ANYTHING....ONLY WHEN YOU CHOOSE TO VALUE YOUR PRODUCTS


Sunday, February 17, 2013

NINI HASA MAANA YA UJASIRIMALI?

NAJUA UMESIKIA MARA NYINGI NA TAFSIRI NYINGI SANA KUHUSU UJASIRIAMALI!

YAMKINI UNAWEZA KUWA NA MAANA SAHIHI AU MAANA DHAIFU!!

LAKINI SASA HAPA NATAMANI UTOE MAONI YAKO HASA JUU YA MAANA UNAYOIFAHAMU WEWE KUHUSU UJASIRIAMALI NA HAPO MWISHONI TUTAONA TAFSIRI IPI INATUFAA KATIKA UHALISIA NA MATUMIZI RAHISI KATIKA MAISHA YETU!!

KARIBU UTOE MAONI YAKO!!!!

Monday, February 4, 2013

JIHADHARI MJASIRIAMALI#.....UTAPELI MPYA UMEINGIA MJINI!!

WAELEWE MATAPELI WALIOKUBUHU HAPA DSM....IMENITOKEA MM LEO 02/02/2013 KWA
MARA YA PILI


Kuna utapeli fulani unaendelea Tanzania na inaelekea wanaoufanya wamefanikiwa

sana na wanaendelea kufanikiwa kwani ni wa muda mrefu sasa. Nadhani matapeli

hawa wanatumia ujinga wetu maana sisi sio watu wakutafuta sana usahihi wa mambo

kabla ya kusema au kutoa maamuzi, pamoja na ujinga wetu wa kutaka kufanikiwa kwa

haraka kwa njia yeyote ile hata kama hatujafanya kazi na bila kutumia akili. Utapeli huu

sio mwingine bali ni ule wa wale watu wanaompigia mtu simu wakijifanya wanakujua

kabisa na wanaweza hata kukupa some backgrounds zako za kazi, ajira au elimu

na meninge hadi ukashawishika kuwa unayeongea naye ni mtu unayemfahamu/

munayefahamiana na hivyo kutokua na hofu na uhalisia wa anachokuambia. Baada ya

hapo wanaanza kukushawishi juu ya kuwasaidia kupata madawa ya kuhifadhi nafaka

kwa madai kuwa mawakala wao ambo wamekua wakizipata toka kwao wameanza

kuleta uswahili hivyo kwa vile unayeongea naye ndio anahusika na suppy, basi ameona

ni vema akutumie wewe “mpendwa anayekujua” ili angalau upate hiyo commission

kubwa ambayo huwapa ho mawakala na mugawane kidogo. Mara nyingi wanasema

wanafanya kazi na shirika la chakula duniani (FAO) au shirika la wakimbizi duniani

(UNHCR) na wako Kigoma.

Zaidi ya mwaka mmoja sasa nikiwa ofisini walinipigia na aliyekua anaongea name

alianza kwa kujitambulisha kama graduate wa kitivo cha uhandishi cha chuo Kikuu

Mlimani na kwamba tulisoma wote mwaka mmoja wakati nikisoma degree ya kwanza

lakini huenda simkumbuki kwa sababu nilikua kiongozi wa fellowship na siwezi kuwa

nakumbuka wote niliokua nawaongoza. Yeye alikua fellowship. Alikua akiongea kwa

kicheko na “bwana yesu” asifiwe nyingi ili kunionesha ni kwa kiasi gani namfahamu

na tunafahamiana. Kwa bahati mbaya wakati ananipigia nilishasikia kwa umbali juu

ya utapeli huo ambao kwa kipindi hicho ndio ulikua umeanza tu na kushika kasi huku

watu wengi wakiwa wamepoteza mamilioni. Hivyo alipoanza kuongea ujinga wake wa

kunipa commission and all that, nilimwambia tu kuwa sina muda wa kujihusisha na

biashara aliyokua “anataka kunisaidia ili nipate pesa za bure”, kwa haraka na bila jasho.

Alikua disappointed sana kwa jibu langu hasa kutokana na muda mrefu alioutumia

kunishawishi nikubali “msaada aliokua ananipa kama mpendwa mwenzake”.

Leo asubuhi majira ya saa nne nilipokea simu kwenye line yangu ya tigo na number

iliyonigia ni 0717-093260. Mtu aliyenipigia alikua anaongea kwa uchangamfu mkubwa

na kwa furaha huku akitaja majina yangu yote na kuniuliza iwapo kwa sasa niko DSM

au nimesafiri. Aliniambia kuwa kafurahi kusikia kuwa niko DSM kwani ndipo zilipo ofisi

zao na kwamba alitaka kuniunganisha zao ili nikachukue mzigo ambao utakua na cha

juu kizuri sana. Nilipoona anaendelea nilimuomba ajitambulishe...akaniambia anaitwa

Lameck na kuwa alishafanya kazi Planet International hapa chuo kikuu. Alipotamka

hivyo nikaanza kupata ukakasi kwani hapajawahi kuwa ofisi ya kampuni hiyo hapa

Mlimani. Nikamuuliza yuko wapi kwa sasa na kwa msisitizo akanijibu kuwa kwa sasa

yuko Serengeti National Park. Nikamuuliza iwapo anafanya kazi na TANAPA..akasema

hapana bali yuko na shirika moja la Kijerumani linalojishughulisha na wanyamapori...na

akijua kuwa niko Chuo Kikuu alitafuta style nzuri ya “kuniingiza alipokusudia” ...maana

alianza kunieleza kuwa shirika lao linafanya “tafiti za wanyama pori katika mbuga

yetu ya Taifa kubwa sana”. Bado nikiwa najaribu kuunganisha “idadi ya nukta kadhaa”

akaniona mjinga sana na kuanza kunielezea jinsi wanyawa walioko Serengeti wanavyo

migrate kila mwaka kwenda Kenya.....na kuwa wanahama wengi kama elfu mbili

hivi...(nikapata nukta nyingine)..then nikaingilia na kumsaidia kuwa hawavuki kwa

maelefu bali ni zaidi ya milioni moja wanahama na kurudi kila mwaka. Pomaja na utafiti

kazi nyingine wanayofanya ni pamoja na kutoa chanjo kwa wanyama hawa maana

wanaporudi wanakua wamerudi na magonjwa toka Kenya.

Hapa ndipo alipopotea njia zaidi kwani kati ya jambo ninalolijua kwa mapana

kidogo ni hii movement ya wild beasts, zebra na wengine walioko Serengeti .

Nikamuonesha kushangaa kuwa wanawezaje kuwapa chanjo

namna hii (na kumuonesha najua chanjo ni nini nikajifanya mhaya kidogo na kutamka

vaccination)...akaanza kujichanganya kuwa wao wana njia tatu za kutoa chanjo

maana ni kweli kuwa wanyama ni wengi...kwanza wanatengeneza majosho/mabwawa/

madimbwi ambayo wanaweka dawa na hiyo wale wanyama wanapokua wanarudi

wanatumbukia na hivyo automatically wanakua wamepata chanjo. Hapa akachemka

zaidi...nikamuuliza hivi kuogesha ng’ombe kwenye majosho ni chanjo au ni kuua

kupe na viroboto? Nikamuuliza kuna chanjo inafanyika juu ya ngozi?...alipoona hana

majibu akauma maneno mawili-matatu halafu akasema njia ya pili wanayotumia

ni kuwakamata wale wakubwa kama tembo na wengine na kuwapiga sindano za

chanjo....nikajizuia kucheka. Alipoona swali lingine linafuata kabla hajaanza kuningiza

kwenye “undani/details za deal” lenye commission ...akaomba udhuru kidogo kuwa

boss wao kaingia ofisini mara moja na hivyo atanipigia baadaye kidogo...akakata simu

na ukawa ndio mwisho wa mawasiliano

Alipokata simu tu nikamtext kuwa angeendelea tu na ujinga wake maana nawafahamu

vema na wanachokifanya...na huo ukawa ndio mwisho wa ile number kupatikana

hewani baada tu ya ujumbe wangu kuwa delivered.

Ushauri Kidogo:
• Unapojikuta kwenye mazingira ya mtu kujitambulisha kwako kwa nguvu kubwa huku

ukiwa humfahamu, mpe nafasi ya kuongea

• Unapojikuta kwenye mazingira ya kudanganyika kuwa unaweza kunufaika na kupa

utajiri kirahisi kwa mtindo wa ki_DECI_DECI au kimuujizaujiza, usichanganyikiwe

na kuanza kuutazama huo muujiza kama ndio umeshakufikia. Utafanya la muhimu

sana iwapo utaruhusu akili yako kufanya kazi na kutafakari vema kila unachokiona

au kukisikia

wanyama wengi

Kama unaweza, ni vema kurecord mazungumzo ambayo una wasiwasi nayo

• Kama unaweza, una nafasi, na una matumaini kuwa polisi wanaweza kuwa na

msaada kwenye hili, basi wasikilize watu hawa na kutafuta msaada wa polisi kwani

utaokoa na wengine wasidanganyike

• Tambua tu kuwa watu hawa wana mtandao mkubwa sana na mara nyingi

wanafanya mambo yao wakiwa na taarifa za kuwatosha na wamejipanga. Unaweza

ukawa kwenye mstari mwembamba sana unaotofautisha ukweli na uongo

• Kwa nini bado makampuni ya simu yanaruhusu simu kutumika ikiwa haijasajiliwa?

Na kama imesajiliwa, je wale wanaoandikisha hizi simu, wana ujuzi wowote wa

kugundua kitambulisho halali na ambacho ni fake watu wanavyovitumia kusajilia

simu zao?

Ufahamu na Akili tuliyonayo ukitumika vema bil haraka ya mafanikio tunaweza kukabiliana
na changamoto nyingi za kitapeli tunazokumbana nazo

IMEANDIKWA NA
MATHEW MNDEME a.k.a MM