Monday, September 30, 2013

NJOO UWE SEHEMU YA HISTORIA HII YA TANZANIA NA JOHN LISU!!

UKO HAPA DVD LIVE RECORDING
 NA JOHN LISSU,
06/10/2013,CCC-UPANGA, DAR ES SALAAM, TANZANIA.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE;
SALAM TANZANIA!

Shalom Dar es salaam, Shalom Tanzania!
Ndugu wanahabari na watanzania wote kwa ujumla!
Naamini tuko salama na tunaendelea na shughuli zetu za kila siku alizotupatia Mungu wa mbinguni, tumshukuru Mungu sana kwa Amani na utulivu aliotupa na tuendelee kumuomba ili atuepushe na kila aina ya dhahama na uharibifu wa Yule adui!
Kama tulivyosikia hivi karibuni, yale yaliyotokea nchi jirani ya Kenya, kwa hakika tunawapa pole sana kwa mkasa huo, pole kwa wale waliowapoteza wapendwa wao na wale waliojeruhika tunawaombea wapone haraka, tunaamini hekima ya Mungu itakuwa juu ya serikali yao kushughulikia jambo hilo kikamilifu.
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai, hata sasa tunapoende kumalizia robo ya tatu ya mwaka 2013, tumeshuhudia mambo mengi sana mwaka huu ya kila aina, yapo yale yalionza kwa mara ya kwanza na mengine yamekuwa ni mwendelezo tu wa yale yadumuyo au yalioyaanza hapo kale, tumeshuhudia michezo mbalimbali na vipaji lukuki vikiinuka na kuimarika katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, na kwa yote mema na mazuri tunampa Mungu Utukufu kwa hakika!


UTANGULIZI JUU YA JOHN LISU;

John Lisu ni mmoja wa waimbaji/Waabudishaji wanaoheshimika katika Tasnia ya muziki wa Injili kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kukuza na kuendeleza muziki wa Injili nchini Tanzania na nje ya Nchi. Nyimbo nyingi alizozitunga na kuziimba zimekuwa zikitumika katika makanisa mbalimbali kama nyimbo za kusifu na kuabudu; pia waimbaji wengine waliokua wakiimba naye wameweza kukua na kufikia uwezo wa kuwa waimbaji wa kujitegemea. John Lisu pia ametia hamasa kubwa miongoni wa wanamuziki wa Injili kuanza kufanya muziki wa live. John Lisu ameweza kufanya tours za ndani ya Tanzania, Africa na Bara la Ulaya kwa ajili ya huduma.
CHRISTINA SHUSHO

John Lisu anategemea kufanya Project II ya Live recoding inayojulikana kama "UKO HAPA" baada ya project ya kwanza ya Jehova yu hai kufanya vizuri sana. Tamasha litafanyika ndani ya ukumbi wa City Christian Centre (CCC) Upanga tarehe 6 Octoba 2013, kuanzia saa 8. mpaka saa 2 usiku.
PAUL CLEMENT

 Tamasha litasindikizwa na waimbaji nguli kama Christina Shusho, Neema Gospel Choir, Paul Clement, Pastor Safari Paul, Bomby Johnson Waimbaji wote wamethibitisha kuwepo. 

BOMBY JOHNSON

VENUE:
City Christian Centre (CCC) mkabala na chuo kikuu cha mzumbe
Si mbali saana kutoka Diamond Jubilee
MIRIUM LUKINDO WA MAUKI


USAFIRI (basi zilizobandikwa matangazo ya tamasha) utakuwepo kutoka posta mpya kwenda ukumbini kuanzia saa saba na nusu mchana kwa bei ya kawaida.
PASTOR SAFARI PAUL

HABARI NJEMA-MUHTSARI!!!!!

Sasa kwa mara pili nchini Tanzania, mwimbaji WA NYIMBO ZA INJILI na mwabuduji JOHN LISSU wa jijini Dar Es Salaam, atakuwa anafanya Ibaada kubwa ama Tamasha la kusifu la Kuabudu(LIVE PERFORMANCE), litakalorekodiwa moja kwa moja (DVD LIVE RECORDING) lenye jina “UKO HAPA” (Yaani Mungu na Uwepo wake).
Tamasha hilo litafanyika jumapili ya Tarehe 6, Octoba 2013  katika Ukumbi mkubwa wa kisasa wa Kanisa la City Christian Centre (CCC)- Upanga, mkabala na Chuo Kikuu Mzumbe – tawi la Dar es salaam, kuanzia saa nane mchana.
Tunataraji watu 5000 kuwa sehemu ya tamasha hili la kipekee,Utakuwa sehemu ya tamasha hilo kwa tiketi ya 10,000/= (kawaida), 20,000/= (VIP) na 3000/= (Watoto);
na Kwale watakaohitaji tisheti maalum za tukio hilo, basi zinapatikana kwa kati ya 12,000-15,000/=, wewe wasiliana tu na (0713905118)
NELLY-MKE WA JOHN LISU


VITUO VYA KUUZIA TIKETI;
1.   MWENGE – Tarakea duka la Kanda
2.   KINONDONI – DPC
3.   MLIMANICITY – Silverspoon Restaurant
4.   KARIAKOO – Mbogo Shop
5.   UKONGA BANANA – KWA GIDO
6.   POSTA - DUKA LA MSAMA

T-SHIRTS

-T-shirts maalumu kwa wanaume na wanawake zinapatikana katika vituo vya kuuzia tiketi kwa bei ya elfu kumi, mpaka elfu 15(kutegmeana na aina).

N.B; Kwa tiketi ya VIP, mnunuzi atajipatia na Audio CD ya John Lissu ya “Uko Hapa”

USAFIRI UTAKUWEPO!!
Siku ya tamasha kutakuwepo usafiri kutoka Posta Mpya mpaka CCC-Upanga,eneo la tukio, hivyo kama wewe ni mgeni na hupafahamu mahali hapo, basi utakachotakiwa kufanya ni kupanda magari toka ulipo mpaka posta mpya kabla ya saa nane,na hapo utayakuta mabasi yenye mabango ya Tamasha, basi utajongea humo na hapo utawezeshwa kufika eneo la tukio, muhimu ni kuzingatia muda!

MUHIMU SANA!!

JOHN LISU NA TIMU NZIMA WAKIWA MAZOEZINI


Tamasha hili ni muhimu sana kwa Tanzania, hasa ukizingatia JOHN LISSU ni mmoja wa waimbaji wa kwanza kuimba live kila mahali anapoalikwa na ni mwimbaji wa kwanza binafsi kufanya LIVE DVD RECORDING pale Ubungo plaza, na ile ya kwanza iliitwa “JEHOVA YU HAI” na sasa anafanya LIVE RECORDING kwa viwango vingine bora zaidi, maana Mungu hutupa hatua moja zaidi kila siku.
Ni muhimu kwa kila mtanzania kujivunia kipaji na tukio hili muhimu katika historia, njoo umwabudu na kumsifu Mungu pamoja, Njoo ujifunze, Njoo umuunge mkono mtanzania mwenzako na njoo uje ufanyike sehemu ya Historia hii kwa Utukufu wa Jehova.
NEEMA GOSPEL CHOIR-KWAYA PEKEE ITAKAYOSHIRIKI "UKO HAPA"


MWALIKO MAALUM;
Kipekee Ninapenda kuwakaribisha wachungaji, mitume, manabii, wainjilisti, waalimu na viongozi wote wa makanisa na huduma mbalimbali, ninawakaribisha viongozi wote wa kisiasa na kijamii kutoka serikalini na vyama vya siasa vyote, ninapenda kuwakaribisha wanaharakati na wanataaluma wote, ninapenda kuwakaribisha waimbaji wote wa nyimbo za injili na wanasanaa wote, ninapenda kuwakaribisa wanafamilia wote, asiwepo wa kubaki nyuma, ninapenda sasa kukukaribisha wewe unaesoma hapa, naam nisaidie kumkaribisha na mwenzako na yeye aje na mwenzake, kimsingi tukio hili ni letu wote bila kujali kitu chochote, njooni tumsifu na kumwabudu Bwana na Mungu hataacha kuibariki Tanzania!
EMMANUEL NDIYE ATAKAYEMPIGIA JOHN LISU LEADING GUITOR


SHUKRANI;
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Hakneel Production (Wadhamini wakuu), na Jonn Lissu na timu nzima ya maandalizi; Kanisa la CCC-Upanga; vyombo vya habari hususani Praise Power na WAPO Radio; Clouds TV kupitia CHOMOZA na Clouds Radio kupitia GT; Sibuka Tv kupita Gospel Hits; Bloggers hususani Christian Bloggers, magazeti na vyombo vingine vyote vya habari! Shukrani hizi zimfikie kila mtu mmoja mmoja aliyetoa mchango wa mawazo, fedha, ushauri, maombi, ubunifu, yaani mchango wowote wa hali na mali na Mungu awabariki nyote!
MIRIUM LUKINDO WA MAUKI


MUHTASARI MKUU;
Tukio; TAMASHA LA KUSIFU NA KUABUDU, LITAKALOREKODIWA
(DVD LIVE RECORDING CONCERT)
Mhusika; JOHN LISSU
Jina: “UKO HAPA”
Mahali; UKUMBI WA KANISA LA CITY CHRISTIAN CENTRE (CCC)- UPANGA
Lini; 06TH OCTOBA, 2013
Muda; KUANZIA SAA NANE MCHANA
Kiingilio; Tsh 10,000/= (kawaida); 20,000/= (VIP) na 5000/= (Watoto)

Wasindikizaji; CHRISTINA SHUSHO, MIRIUM LUKINDO, PASTOR SAFARI, BOMBY JOHNSON, NEEMA GOSPEL CHOIR-AIC Chang’ombe na PAUL CLEMENT.

Mengineyo; USAFIRI UTAKUWEPO TOKA POSTA MPAKA CCC-UPANGA na Unaweza kujipatia Tisheti pia.
Wahusika; WATU WOTE MNAKARIBISHWA!


UKIPATA HABARI HII USIACHE KUMSHIRIKISHA NA MWENZAKO, NAAMINI HAUTAKOSA TUKIO HILI MUHIMU LA KIHISTORIA KATIKA NCHI YA TANZANIA KWA UTUKUFU WA MUNGU!!





KWA PICHA NA TAARIFA ZAIDI;


http://www.youtube.com/watch?feature=player_detailpage&v=blz0PKQ6QNU




MAWASILIANO:
O713 240 397 – JOHN LISU
0713 905 118 –PROSPER MWAKITALIMA – EVENT MANAGER
0713 883 797 - FREDY CHAVALA - PUBLICITY


Imetolewa na;
Fredy E. Chavala <King Chavala (MC)>
Publicity Manager
+255 713 883 797
On Behalf of The Organizing Committee

No comments:

Post a Comment